Blogger Widgets KASEJA, NGASA, KAPOMBE NA KAZIMOTO WAULA | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Sunday, October 7, 2012

KASEJA, NGASA, KAPOMBE NA KAZIMOTO WAULA


WACHEZAJI wanne wa mabingwa wa ligi kuu Bara, Simba wakiwemo  Nahodha Juma Kaseja, Mrisho Ngasa, Shomari Kapombe na Mwinyi Kazimoto wanatarajiwa kuonekana katika nchi mbalimbali duniani baada ya wasifu wao na baadhi ya picha cha michezo yao kurekodiwa kabla ya kurushwa na kituo cha Televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini.
 Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga ameiambia kikwatojr.blogspot.com kwa njia ya simu ambapo ameeleza kuwa zoezi hilo limewezeshwa na wadhamini wa timu hiyo kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro na kuongeza kuwa ni hatua nzuri ya kuelekea mafanikio ya kupata timu za kucheza nje ya nchi kwa wachezaji hao. 
kama mjuavyo SuperSport inaonekana duniani kote hivyo wachezaji wetu watapa kuonekana na vilabu mbalimbali na kwa njia hiyo wanaweza kupata timu za kucheza katika sehemu tofauti duniani,”alisema

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.