(hao pia ni mingoni mwa washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya unyanyasaji yanayoendeshwa kwa ufadhili wa Shirika la INUKA na SWAT )
SHIRIKA la Mfuko wa taifa wa Bima ya afya limeshauriwa kuongeza ufanisi kwa kuboresha huduma zake zaidi ili kuondoa usumbufu na malalamiko kwa wanachama wake.
Hayo yalielezwa na washiriki
wa mafunzo ya siku tatu ya unyanyasaji yanayoendeshwa kwa ufadhili wa Shirika
la INUKA na SWAT na kufanyika kwenye ukumbi wa kanisa la Elimu
Pentacost la Masuguru Mjini Muheza.
Washiriki hao ambao wengi
wao ni walimu, walilalamika kuwa huduma za bima ya afya bado hazijatengemaa
vema na kwamba kuna haja kwa wahusika kujipanga na kuhakikisha kuwa wanachama
wake wanapata wanachotarajia ipasavyo.
Walidai kuwa licha ya
kukatwa fedha nyingi kila mwezi lakini fedha wanazotozwa haziendani
na huduma zinazotolewa jambo walilolieleza kuwa linawafanya wakate tama
na kujutia michango yao.
Kwamujibu wa washiriki hao
ni kwamba wanalazimika kutoa michango yao kila mwezi lakini hawapati huduma
wanayotarajia na badala yake wanapokwenda hospitali wanatakiwa kulipia
dawa na vipimo vingine na hivyo kupata gharama kubwa.
Mambo mengine yaliyojitokeza
kwenye mafunzo hayo ni pamoja na malalamiko zidi ya Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Muheza kudaiwa kutoa siri kwa
kuwataja kwa waharifu watu wanaojitoa kupeleka taarifa za makosa
hayo katika ofisi zao.
Aidha washiriki hao
walilalamikia unyanyasaji katika jeshi la polisi.Mahakama pamoja na
watendaji mbalimbali katika maofisi ya serikali na binafsi na kwamba
wamekuwa wakipata manyanyaso kwenye ajira kwa upendeleo wenye mazingira ya
rushwa.
Awali mkufunzi wa mafunzo
hayo Nestory Ngwega alitumia muda mwingi kueleza haki za msingi za binaadamu
ambazo zisipofuatwa ndipo tendo la unyanyasaji hutokea na kwamba haki hizo zipo
kwenye makundi mawili ambayo ni haki ya kikatiba na ile ya kibinaadamu ambayo
haiondolewi na mtu yeyote Yule kwa nafasi yake ama uwezo wa kifedha.
Mengine yaliyojadiliwa
katika mafunzo hayo ni unyanyasaji ndani ya familia na kwa wanandoa
pamoja na vyanzo vyake na jinsi ya kukabiliana navyo.
No comments:
Post a Comment