Blogger Widgets SIRI YANGU YA KUTUMIA LAFUDHI YA KIMASAI | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Saturday, October 27, 2012

SIRI YANGU YA KUTUMIA LAFUDHI YA KIMASAI



 HATIMAYE msaani maarufu wa vichekesho nchini, Gilliady Severine a.k.a Masai Nyotambofu, ametoa siri yake ya kutumia lafudhi ya jamii ya Kimasai katika kazi yake ya sanaa ya maigizo na vichekesho.
Akizungumza na blog hii jijini hapa juzi, Nyotambofu alisema kuwa, yeye aliamua kutumia lafudhi ya Kimasai baada ya kubaini kuwa ni ngumu na hata waliyokuwa wakijaribu kuitumia katika sanaa mbalimbali, hawakuweza kukidhi mahitaji ya lafudhi ya lugha hiyo. Msanii huyo amekuwa akisikika katika matangazo mbalimbali yanayorushwa na vituo vya radio hapa nchini, hasa ya uhmasishaji wa kuacha pombe, yaani ‘ulevi noma’ lilitolewa na Idara ya Ustawi wa Jamii wakishirikiana na Jeshi la Polisi. “Ndugu mwandishi, niliamua kutumia lafudhi ya Kimasai, kwani nilishafanya utafiti na kubani kuwa, lugha hii ni ngumu kuiga, pia niliangalia wasanii ambao walikwisha kujaribu kuitumikia lafudhi ya Kimasai, nikaona hawajakidhi kabisa ndipo nikaamuua kuitumia na mpaka sasa najivunia nimeweza,” alisema Masai Nyotambofu. “Hata hivyo, ilibidi niongeza juhudi na kujituma katika kuitumia lafudhi hii baada ya kupewa zawadi ya fimbo na mgolole na wazee katika Wilaya ya Ngorongoro, baada ya kuona nimeweza kuimudu lafudhi yao tofauti na wasanii waliokwisha kuwahi kuitumia katika maigizo na muziki,” alisema na kuongeza: “Kilichonitia moyo na kuongeza juhudi katika kutumia lafudhi hii, mwaka 2010 nilikwenda Ngorongoro kufanya onyesho na mwanamuziki Banana Zoro, ilikuwa sikukuu ya wafanyakazi, ndipo wazee wa Kimasai wakaridhika na kazi yangu wakanizawadia huo mgolole na fimbo, mpaka sasa ndivyo ninavyovitumia,” alisema Masai Nyotambofu. Msanii huyo maarufu, ambaye ni Muha kutoka Kigoma, yupo jijini Mbeya kwa ajili ya kurekodi vipindi vya ‘Vituko Show’ vinavyorushwa na kituo cha televesheni ya Channel Ten.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.