Blogger Widgets warembo wa bongo muvi wajichafua ili wajisafishe | Mfaume Kikwato JR

PALACE HOTEL

PALACE HOTEL

Vumbua Hazina chini ya kizibo

Vumbua Hazina chini ya kizibo
+255788788218

BAYPORT

BAYPORT
KOPA BAYPORT

Tuesday, October 16, 2012

warembo wa bongo muvi wajichafua ili wajisafishe

wema sepetu akiwa na mwenzake ant ezekiel mbele ya wandishi wa habari wakiomba razi kwa picha zao za kuonesha hali ya utupu  walizo pigwa wakati wa tamasha la serengeti fiesta


Awali ya yote tunawapongeza kwa jitihada zenu za kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu kazi zetu za Filamu na Sanaa kwa ujumla.
Kiukweli sisi tukiwa sehemu ya wahusika  katika Wahusika wengi ndani ya tasnia ya Filamu Tanzania, hatuna hiari isipokuwa ni lazima kuwapongeza na kuwashukuru katika harakati na kwa mchango wenu wa kukuza tasnia ya filamu kupitia  habari mbalimbali zinazohusu tasnia ya hii pamoja na kwamba ni wajibu wenu.
 Lakini Pongezi zaidi za dhati tunaziwasilisha kwenu  leo hii (15 .10.2012) moja kwa moja ,kwamba kazi yenu  ya uandishi imetusaidia kwa kiasi kikubwa kufikia maendeleo haya machache  tuliyo nayo, lakini mchango wenu pia si umetusaidia kupata mafaniko tu lakini pia umetusaidia kujifunza mambo  mbalimbali kuhusu filamu za wenzetu na pia kutuonya katika mambo mbalimbali  .
 Ndugu Waandishi wa Habari, tasnia ya filamu ni moja kati ya fani zinazokuwa kwa kasi na kuleta mafanikio  na maendeleo ya baadhi ya vijana wengi wa Tanzania, kutokana na hilo tasnia imekuwa ni moja kati ya maeneo mapya ya ajira kwa raia wa Tanzania na serikali yao kwa ujumla, ni eneo ambalo kwa kiasi kikubwa limechukua rika na jinsia zenye elimu tofauti kwa kusudio la uzalishaji wa filamu bila ya kuzingatia elimu ya muhusika .
 Ndugu Waandishi kutokana na kukua huko, tasnia hii imezalisha Wasanii wa Tanzania ambao sasa wana majina yanayosikika  kila pembe ya nchi yetu, hali hii  imesababisha kuvutia vyombo vya habari kutaka kujua Wasanii wetu wanafanya nini sehemu mbalimbali walizopo.
 Ndugu  Waandishi  mtakumbuka  kwamba  hivi  karibuni kulikuwa tamasha la muziki lililojulikana Serengeti Fiesta ambalo liliandaliwa  na kampuni ya Prime Time Promotion kwa pamoja na Clouds Entertainment za mjini Dar es Salaam,
 Katika matamasha hayo Wasanii kutoka Bongo Movie Club tulialikwa kama wasindikizaji ili kupamba matamsha hayo katika sehemu yalikofanyika. Katika tamasha la Serengeti Fiesta lililofanyika Dodoma baadhi  ya  Waandishi  ambao walihudhuria tamasha lile walifanikiwa kupiga Picha tofauti tukiwa jukwaani.
Baadhi ya picha zilizopigwa katika tamasha lile hazikuwa nzuri kuoneshwa katika hadhara za watu iwe nyumbani au katika vyombo vya habari. Lakini katika hali isiyotarajiwa picha zile zilisambazwa katika mitandao mbalimbali pamoja na kutolewa  katika baadhi ya magazetNdugu Waandishi tunapenda kujulisha umma wa Tanzania kwamba hatujakusudia kupiga tukiwa vile isipokuwa ni mambo ya kiutaalamu katika upigaji wa picha ambapo imechangia kuonekana vile lakini pamoja na upigaji wa picha kuwa wa kiutaalamu zaidi , kwa sababu nyingine ni ya jukwaa lenyewe lilikuwa  refu  zaidi sana.
 Nasi tumeumia sana mioyoni mwetu baada ya kuonekana kwa picha zile kwa sababu sisi kama Wanawake katika jamii tuna Wazazi, ndugu, jamaa , marafiki pamoja mashabiki  mbalimbali wa kazi zetu ambao wanatuheshimu kuliko baadhi ya watu wanavyofikiria , kiukweli hatujafurahia na tumeumia  sana.
 Ndugu Waandishi  wa habari pamoja na yote yaliyo tokea tunachukua nafasi hii kuomba msamaha  kwa Wizara Habari Utamaduni Vijana na Michezo  na taasisi zake , Shirikisho la Filamu Tanzania,Bongo Movie Club na Wadau wake, Familia zetu  na jamii kwa ujumla kutokana na picha zilizopigwa tukiwa katika onesho  la fiesta  ambazo zimesambazwa katika vyombo vya habari na mitandao mbalimbali.
Watanzania  na hasa Wanawake wenzetu kwa kadhia hiyo na tunaahidi kwamba jambo hilo halitajirudia tena  aidha pia tunaomba waandishi sasa waanze kutazama mambo mazuri tuliyoyafanya  na si kutuwinda kwa mabaya kwani sisi ni binadamu na wala si malaika .
 Lakini pia tunapenda kutumia nafasi hii kuvijulisha vyombo vya habari kwamba kuanzia leo tunataka visitumie tena picha hizo na kuziondoa katika mitandao yao  kwa sababu tunaamini kwamba hazileti  mafunzo yoyote katika jamii zaidi tu kwamba zinazidi kupotosha jamii, na ukizingatia lengo kuu la vyombo vya habari kuelimisha na kuburudisha pia.
 Mwisho ni matumaini yetu kwamba tutapewa ushirikiano katika mambo mbalimbali yanayotuhusu na tasnia ya filamu kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.